Jumatatu 10 Novemba 2025 - 21:25
Hamas Yapokea Uamuzi wa Mahakama ya Uturuki

Hawzah/ Harakati ya Hamas imeitaja tangazo ya hati ya kukamatwa kwa maafisa 37 wa Israel, akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, kuwa ni hatua ya haki.

Kwa mujibu wa Idara ya Habari za Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Hamas imepongeza uamuzi wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Istanbul kwa kutoa hati ya kukamatwa maafisa 37 wa utawala wa Kizayuni, wakiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kwa tuhuma za “uhalifu dhidi ya ubinadamu” na “mauaji ya kimbari.”

Katika taarifa rasmi ya Hamas imesemwa: “Tunapongeza hatua ya Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Istanbul kwa kutoa hati ya kukamatwa Waziri Mkuu mhalifu wa utawala wa kinyakuzi, Benjamin Netanyahu, pamoja na mawaziri wa ulinzi wa zamani na wa sasa wa utawala huo, Yoav Gallant na Yisrael Katz, wakiwemo maafisa wengine 36 wa Kizayuni.”

Hamas imeeleza kuwa uamuzi huo ni kielelezo cha msimamo wa haki na utu wa Uturuki, na ikasisitiza kwamba ni ishara ya mshikamano wa kweli na watu wa Palestina mbele ya mauaji ya kimbari na uhalifu unaoendelea wa Israel.

Katika sehemu nyingine ya taarifa hiyo, Hamas imezitaka nchi nyingine duniani kuchukua hatua kama hiyo dhidi ya maafisa wa Israel na kuwawajibisha kwa uhalifu wao mkubwa dhidi ya ubinadamu.

Kwa mujibu wa agizo la Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Istanbul, hati za kukamatwa zimetoa amri dhidi ya maafisa 37 wa utawala wa Kizayuni, akiwemo Netanyahu, kwa sababu ya vitendo vyao vya kimfumo dhidi ya raia wasio na hatia wa Ghaza na mashambulizi dhidi ya msafara wa kimataifa wa kutoa msaada wa “Samoud.”

Aidha, Ubalozi wa Palestina mjini Ankara, katika taarifa nyengine, umeukaribisha uamuzi huo wa Uturuki, na kuutaja kuwa ni hatua ya kishujaa inayotegemea ushahidi ulio wazi wa mauaji ya maelfu ya raia, wakiwemo wanawake na watoto, uharibu wa makusudi wa hospitali na miundombinu, na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Ghaza.

Katika taarifa hiyo ya ubalozi pia imekumbushia tukio la kusikitisha la hivi karibuni, yaani kuuwawa mtoto wa Kipalestina mwenye umri wa miaka sita, Hind Rajab, mikononi mwa wanajeshi wa Israel, jambo lililo umiza dhamiri ya dunia.

Balozi wa Palestina amezitaka nchi na taasisi za kimataifa zichukue hatua kama hizo kwa ajili ya kuwashtaki wahalifu wa kivita wa Israel na kuwafikisha mbele ya haki.

Mwisho wa taarifa hiyo imeeleza kwamba; Serikali ya Palestina itaendeleza mapambano yake ya kisheria na kidiplomasia katika jumuiya zote za kimataifa ili kuwasaka na kuwaadhibu wahalifu wa utawala wavamizi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha